Neno la Mungu ndiyo chemchemi ya nguvu za kiroho, ndilo hututia moyo, na ndilo hutuhekimisha. Bila Neno la Mungu, mtu yeyote angewezaje kuijua njia ya Mungu ya wokovu? Njia ya wokovu haiwezi kutokana na dhana au mawazo yetu binafsi. Biblia inafunua wokovu ni kwa imani katika Kristo. Kwa hiyo tunaposoma Biblia, tunafanywa wenye hekima hata kufikia wokovu. Hata hivyo ni muhimu kujua kuwa hiyo Imani, huja kwa kusikia neno la Mungu. Kusikia ni tofauti na kusikiliza. Kusikia inahusisha kuelewa na kulitumia neno katika maisha ya kila siku. Ndiyo maana ni muhimu kuwa na mahali sahihi na penye kuaminika ambapo mtu anaweza kupata fafanuzi kwa maswali ambayo hujitokeza pale tunapoyasoma maandiko ili imani zetu zipate kuthibitishwa na kuimarishwa na hatimaye kuufikia wokovu.
0 Comments
Add CommentAdd your comment
To add a comment you need to login or register.